UPDATES ZA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014:-Wilaya ya Muleba,Buhigwe na kwingineko. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 15, 2014

UPDATES ZA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014:-Wilaya ya Muleba,Buhigwe na kwingineko.

Takwimu uchaguzi: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Takwimu ya mambo yaliyotokea wakati wa kampeni za Uchaguzi Serilali za Mitaa.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Mkoa wa Tabora unaongoza kwa ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ukifuatiwa na Kagera wakati Shinyanga na Mbeya wakifanya vizuri.

Kwa upande mwingine takwimu zinaonyesha kuwa kukosekana kwa mwamko wa kisiasa 19%, kampeni kuisha baada ya muda 18%, ratiba za kampeni kuwa wazi 12%, rushwa kwa wapiga kura10%, huku kampeni kuzuiwa na mamlaka 1% na vitisho kutoka kwa watu wasio vyombo vya dola 1%.


MATOKEO. 

MULEBA.

Matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana Desemba 14,2014, nchini kote, yanaonesha kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kinaongoza katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kwa kupata viti 52 huku CHADEMA kikiwa na viti 32 katika ya vito 166 vinavyowaniwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba ,Bw Josephat Mkude amesema matokeo hayo yanakifanya Chama cha Mapinduzi kiwe na viti 65 baada ya kupata Wenyeviti 13 waliopita bila kupingwa wakati wa kura za maoni.

Bw Mkude amesema wilaya ina vitongoji 752 na kwamba ukusanyaji wa matokeo unakwenda taratibu ambapo amesema kufikia leo Desemba 15,2014, majira ya Saa 12 jioni zitakuwa zimepatikana takwimu nyingine za matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika kwa amani na utulivu.

Hata hivyo Msemaji wa kambi ya upinzani kupitia Ukawa Bw Hamis Yusuf ambaye ni Katibu wa Chadema wilayani humo amesema wamekosa ushindi katika uchaguzi huo kwa kuwa sera ya Ukawa haikueleweka kwa wagombea wao.

BUHIGWE.

Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imepokea matokeo ya vijiji 16 ikiwa ni sehemu ya Matokeo ya awali ya uchaguzi katika wilaya hiyo

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Simon Mumbee amesema kati ya vijiji hivyo, kwa nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji, Chama cha Mapinduzi kimepata viti 11, NCCR Mageuzi viti vitatu wakati Chadema na CUF kila chama kimepeata kiti kimoja.

Amesema katika nafasi za wenyeviti wa Vitongoji, CCM kimepata viti 43, NCCR na Chadema vimepata viti 10 kila chama huku Chama cha Wananchi CUF kikipata viti vitatu.

Bw Mumbee amesema kwa upande wajumbe wa Halmashauri za Vijiji, CCM kimepata wajumbe 101, NCCR Mageuzi wajumbe 18, Chadema na CUF wajumbe 16 kila chama.

Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe amesema katika nafasi za viti maalum wajumbe Halmashauri za Vijiji CCM kimepata wajumbe 64, Chadema 12, NCCR wajumbe 6 ambapo amesema bado wanaendelea kupokea matokeo ya vijiji vingine.


Akataa kusaini: Mtaa wa Katoma Geita Mjini wananchi wamekesha kusubiri matokeo.Mgombea wa CCM ameshindwa na amekataa kusaini matokeo.
 
Mabomu yatumika: Jeshi la Polisi limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi mkoani Mwanza katika maeneo ya Pasians, Mji Mwema, Kirumba, Ibungiro na Kitangiri baada ya vurugu wakati wa kusubiri kutangazwa matokeo.

Kijiji cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38

Mbozi; Mtaa wa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44

Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198

Ukonga; Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77

Musoma Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464

Ubungo; Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356

Kinondoni; Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318

Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35

Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8

Kitongoji cha Endulele: CHADEMA 170, CCM 130

Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13

Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35

Arumeru Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130

Ushirombo Mjini: CHADEMA inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4

Moshi Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66

Mbozi Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160

Kata ya Mji Mpya, Morogoro yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa miwili mpaka sasa bado vurugu zimetanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.

Kagondo, Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5

Kufungwa Vituo: Katika maeneo mengi vituo vya upigaji kura tayari vimefungwa huku wananchi wakisubiri kwa hamu kujua matokeo.

Uchaguzi Migombani: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa eneo la Migombani, Segerea jijini Dar umeingia dosari baada ya Afisa Mtendaji Kata ya Segerea kutangaza kusitisha uchaguzi huo kimyakimya bila sababu za msingi ambapo wananchi waliamua kumweka mtu kati mpaka akaruhusu uchaguzi huo kuendelea kwa maandishi. 

Akijitetea afisa huyo alidai kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala kufanya hivyo.

Mazimbu, Morogoro: Eneo la Mazimbu, Moro kimenuka mpaka wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kutuliza ghasia wakati wa zoezi la upigaji kura.

Kawe, Dar: Uchaguzi wadaiwa kuingia dosari baada ya mgombea wa CCM kutoa amri ya vitabu kufungwa kabla ya muda ulipangwa.

Kigogo, Dar: Mgogoro umezuka katika Kituo cha uchaguzi Kigogo jijini Dar baada ya wananchi kudai kuwa baadhi ya watu wamepelekwa kama mamluki eneo hilo kwa ajili ya kugipa kura.

Sokoine-Kibaoni, Morogoro: Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.

Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.

Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.

Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.

Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. 

Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.

Chanzo:-Radio Kwizera/Blog za Jamii.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad