Serikali imejipanga kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ujambazi wa kutumia silaha katika ziwa Tanganyika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 16, 2012

Serikali imejipanga kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ujambazi wa kutumia silaha katika ziwa Tanganyika.

Ziwa Tanganyika pamoja na miji muhimu kando yake

Serikali imesema jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ linaendelea kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ujambazi wa kutumia silaha katika ziwa Tanganyika.

Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga taifa Bw Shamsi Vuai Nahodha amesema watu wenye silaha wanaosadikiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo wamekuwa wakifanya uhalifu katika ziwa hilo. 


Amesema kuwa majambazi hayo yamekuwa yakiwashambulia wavuvi na kuwanyanganya vifaa vya uvuvi na wakati mwingine kuwauwa.

 

Ziwa Tanganyika jinsi inavyoonekana kutoka angani

Mahali Afrika ya Mashariki Nchi zinazopakana Burundi, Kongo,
Tanzania, Zambia Eneo la maji 32,893 km² kutegemeana na kiasi cha mvua Kina ya chini kuanzia 3.5 m Mito inayoingia Lufubu, Malagarasi, Ruzizi Mito inayotoka Lukuga Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB 782 m Miji mikubwa ufukoni Bujumbura, Kalemie, Kigoma.

Wazir Nahodha amesema mnamo mwezi May 2012 ,majambazi yenye silaha za kivita kutoka nchi jirani waliwapola wavuvi katika ziwa Tanganyika,kufanya mauaji na kuwajeruhi askari ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya ujambazi yanayofanywa katika ziwa Tanganyika.


Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 bungeni mjini Dodoma leo bw Nahodha amesema serikali italipatia jeshi la majini, meli na boti za mwendo kasi.


Aidha waziri huyo amesema jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limeanza mpango wa kuimarisha ulinzi wa eneo la nchi kavu katika eneo la ziwa Tanganyika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad